Wednesday, July 27, 2011

Shindano Kwa wajasiriamali wanaochipukia:Tanzania


Chuo Kikuu cha Oxford kinaendesha shindano kwa wajasiriamali wanaochipukia jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujifunza zaidi kuhusu wajasiriamali vijana na mawazo yao. Lengo la shindano ni kujifunza kuhusu ujasiriamali barani Afrika.Tungependa wewe ushiriki. Ukichagua kushiriki, utaandika muhtasari wa kurasa tatu wa wazo la biashara na kufanya uwasilishaji mfupi wa wazo hilo mbele ya kamati ya wajasiriamali sita wa Tanzania.Kuna kamati kadhaa. Kila kamati itawafanyia tathmini waombaji 12 na kuchagua mwombaji mwenye wazo bora la biashara miongoni mwa waombaji hawa 12. Tunakusudia kumzawadia kiasi cha dola za kimarekani 1000 (karibu na Sh. za kitanzania milioni 1.6) kila mwombaji aliyechaguliwa na kamati zao.
Shindano liko wazi kwa mwombaji chipukizi yeyote aliye na umri kati ya miaka 18 na 25 (ikijumuishwa). Shindano liko wazi kwa wajasiriamali walio tayari na biashara na wajasiriamali wanaotaka kuanzisha biashara.
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 29.07.2011. (kama hatutapokea maombi ya kutosha mpaka tarehe hiyo, basi tutaongeza muda wa kutuma maombi, lakini tutawapa kipaumbele wale waliotuma maombi kabla ya tarehe iliyotajwa hapo awali)
Kama ungependa kushiriki shindano hili, tafadhali fanya yafuatayo:
1. Tafadhali andika wazo lako la biashara katika kurasa tatu, kwenye mfumo wa PDF au Microsoft Word.
2. Tafadhali jaza fomu ya maombi kwa kubonyeza hapa. (Mwishoni utapaswa kuambatanisha wazo lako la biashara)
Kama una swali lolote wasiliana nsi kwa barua pepe aspiretanzania@gmail.com.

No comments:

Post a Comment